Campus administration

Prof. Honest P. Ngowi

Principal

Email:This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Prof. Honest P. Ngowi

Principal

Email:This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

Prof. Honest P. Ngowi

Principal

Email:This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.


CHUO Kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam kimefanya mhadhara wa wazi wenye lengo la kutoa uelewa kwa makampuni juu ya wajibu wao kwa jamii kwa kufuata mpango wa maendeleo endelevu ya dunia.

Katika mhadhara huo, profesa Caroline Ditlvet wa shule ya Biashara Norway alifundisha washiriki, ambao ni viongozi mbalimbali wa makampuni na taasisi za kiraia, juu ya uzoefu katika nchi zilizoendelea.

“niwajibu wa makampuni kuelewa  kwa jamii kuhusiana na mpango maendeleo endelevu ya dunia na  mashirikaano kati ya NGOs na makampuni katika kutoa huduma kwa jamii kwa maendeleo endelevu ya duniani. Alisisitiza Prof. Ditlvet  alisisitiza.

Hatua hiyo imekuja kutokana na mahusiano kati ya chuo hicho cha Norway na Chuo kikuu Mzumbe.

"Sisi Chuo Kikuu Mzumbe kutokana na mdharara huu tumeandaa ili kuwakutanisha assis za iraia na makampuni na kubadilishana mawazo lakini pia wanafunzi kupata uzoefu wa kitaaluma katika maendeleo endelevu," Mkuu wa Chuo cha Mzumbe, Profesa Honest Ngowi, amesema.

Amesisitiza kuwa chuo kitaendelea kushirikisha taasisi mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia kwa kufanya tafiti kwa kuwapatia elimu na kufanya tafiti kwa maendeleo endelevu kwenye Nyanja mbalimbali ikiwemo afya, mazingira.

"Nashuri makampuni na asasi za kiraia lazima zishirikiane ili kufanikisha maendeleo kwa pande zote mbili ili zote zinufaike,(win-win situation) katika pande zote mbili zitanufaika siyo lazima kwa kupata fedha, lakini inaweza kusaidia msaada wa kuleta amani katika jamii kwa kushirikiana na asasi za kirai na zinaweza kuleta amani, ulizi na usala. Kwani bila kuwa na amani huwezi kufanya biashara," amesisitiza.

Amesema kuwa vyuo vinatengeza elimu  ambayo itasaidia kuwapa elimu,kufanya tafiti na hivyo ni jukumu la  makampuni na taasisi na mashirika mbalimbali wapeleke mawazo yao katika vyuo waweze kuwasadia nini cha kufanya kwa kuwapa elimu au kuwafanyia tafiti za kuwasaidia kupeleza maendeleo endelevu jamii.

Mratibu wa mhadhara huo, Dkt. Emmanuel Chao,Mhadhiri Mwandamizi kutoka  Chuo Kikuu Mzumbe amesema. Wenzetu nchi wa zilizoendelea watu wao wananunua bidhaa kwa kuzingatia mazingira zilipotengenezwa, ikiwepo swala la kama zinazingatia uhifadhi wa mazingira katika utengenezaji wake.

Lakini pia ni, muhimu kuangalia mambo ya siasa za ulimwengu. Wananchi wengi wameelimika sana kutokana na msukumo wa mabadiliko ya sera za maendeleo ya dunia zinazowekea mkazo swala la dunia endelevu. Kutokana na kuelimika huko, kumekuwa na msukumo kutoka kwa walaji wa bidhaa unaowataka watengenezaji wa bidhaa kuzingatia uendelevu wa dunia.

Kwa kuwa mataifa ya wenzetu yamepiga hatua tunaona vizuri tukashirikiana nao kwa kupeana mawazo, na kuwa na mjadala mpana kama wasomi ili kupata uzoefu utakaoisaidia seriakali pamoja na makampuni yanayofanya kazi nchini.

 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Societies, Bw Francis Kiwanga amesema kuwa mhadhara umekuwa ni fursa kwa asasi za kiraia kwani imewapa nafasi ya kujifunza kuhusu malengo endelevu ya kidunia

Utaratibu wa makampuni kurudisha katika jamii (Corporate social responsibility) ni wajibu wa makampuni kurudiha  huduma kwenye jamii

"Lakini kama taasisi zisizo za kiraia tunawezaje  kushirikiana au kufanya mausiano au ubia na makampuni zinazofanya biashara ili kuweza kuendeleza malengo endelevu ya kidunia," amesema.

Katika mhadhara huo asasi zisizo za kiraia zimejifunza  maono ya kidunia  ni jinsi gani mashirika, taasisi za umma  inafanya katika kuendeleza utaratibu wa makampuni na jamii kuwa na mipango endelevu

"Inabidi tuhakikishe kuwa tunatunza haki za binadamu kuhakiisha tunajali na kutunza mazingira, tunajali maswala ya haki za wafanyakazi na maswala mengine," amesema.

Alishauri kuwa wadau wa asasi zisizo za kiserikali ni  jukumu lao kuwasaidia misaada ya kijamii kwa sababu wao ndiyo wana fahamu vizuri jamii.

Asasi nyingi za kiraia  ili ziweze kurudisha huduma kwa jamii ,zinategemea rasilimali kutoka nje ya nchi lakini wakati umefika rasilimali kutoka nje zitakuja kukata, wito ni makampuni, taasisi na mashirika yatafute ni jinsi gani yatafanya na asasi za kirahia hapa nchini ili kurudisha huduma kwa jamii.

“sisi tuna asasi ambazo zina mifumo. Taasisi ambazo zinafanya vizuri kwa hivyo wanaweza kutumia hizi taasisi kufikia ,malengo yao na  wakati  huo asasi hizi za kirahia na wenyewe zikifikia malengo yao.” Amesisitiza Kiwanga.

                                       Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Prosper Honest Ngowi  akizungumza                                                           mbele ya wadau wakati wa kufungua mhadhara wa wazi kuhusu maendeleo endelevu uliofanyika Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es salaam.

Profesa Caroline  Ditlev Simonsen akiwahutubia washiriki waliojitokeza kusikiliza mhadhara wa wazi kuhusu jinsi gani mashirika yanaweza kuruhisha huduma kwa jamii ili kuleta maendeleo endelevu duniani.

Dkt. Darlene Mutalemwa akimkabidhi Profesa Caroline Simonsen zawadi ya picha ya pundamilia iliyotolewa na Chuo Kikuu Mzumbe huku akimsisitizia kutembelea hifadhi zetu na vivutio vingena kama lengo la kutangaza utalii wa hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa asasi Foundation for Civil Society, Bw Francis Kiwanga akichangia jambo wakati  wa mhadhara huo.

Mratibu wa mhadhara huo, Dkt. Emmanuel Chao,Mhadhiri Mwandamizi kutoka  Chuo Kikuu Mzumbe

 

The training on entrepreneurship was delivered to 50 leather sub-sector members of  small business Society (VIBINDO) at Machinga Complex. It is part of implementing Mzumbe University’s Corporate Strategic Plan on outreach activities.

The aim is to give back to society by way of building capacity and competitiveness of the trainees. It is also part of implementing Memorandum of Understanding (MoU) between Mzumbe University and VIBINDO.

Areas of training include marketing issues, branding and access to finance. The event was organized and facilitated mainly by Msc Marketing students under Mr. Yusuph Zubeir Kashy.

The National Microfinance Bank (NMB) Ilala Branch manager Mr. Seka Urio and Tan Trade Officer Mwanaidi shared some perspectives from their organizations to the trainees. The training was supported by National Microfinance Bank (NMB).

“Outreach activities are very important and among core activities for Mzumbe University. Other core activities include training, research and consultancy. Training at Machinga Complex is one of many similar outreach activities that have been and will be conducted by Mzumbe University in general and its Dar Es Salaam Campus College in particular. Supporters are most welcome to collaborate with us”. Said Prof. Ngowi.

PICTURE: Mzumbe University Dar es Salaam Campus College Principal, Prof. Prosper Ngowi, opening training on leather sub-sector members of Small Business Society. The training was held at Machinga Complex on August 10, 2019.

PICTURE:The National Microfinance Bank Ilala Branch Manager, Seka Urio, giving presentation on opportunities for entrepreneurs related to loan and management.

PICTURE:The Chairperson of Vibindo Society, Gaston Kikuwi, emphasing the important of attending training and implementing the acquired skills.

Mzumbe University will hold its 18th Graduation Ceremonies as follows:

 Main Campus: Friday, 22nd November 2019 at the Graduation Ground starting from 10.00am.

 Mbeya Campus College: Friday, 29th November 2019 at the Graduation Ground starting from 10.00 am.

 Dar es Salaam Campus College: Friday, 6th December 2019 at the Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam starting from 10.00 am.

The ceremonies will be officiated by the Chancellor of Mzumbe University, Hon. Chief Justice (Rtd.) Barnabas Samatta. Candidates who successfully completed their studies and qualified for the award of Certificates, Diplomas and Degrees of Mzumbe University for the 2018/2019 academic year will be conferred their respective awards.

                            For more details,click here

Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam (MUDCC) kimetoa msaada wa vifaa tiba kwa Hospitali ya Taifa Muhimbli kwa ajili ya kusaidia majeruhi wa ajali ya moto baada ya gari la mafuta kupinduka Agosti 9 ,2019 mkoani morogoro.

 Akikabidhi ya vifaa tiba vilivyotokana na michango ya wanajumuiya wa  Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam , Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe Prof. Prosper  Ngowi amesema tumeguswa na janga la moto na hivyo  tumeamua kutoa msaada ikiwa pia ni  sehemu wa kusaidia jamii kama utekelezaji wa mpango mkakati wetu wa  Chuo.

  Amevitaja vifaa vilivyo changiwa na wanajumuiya hao wa chuo  kuwa ni  pamoja na Pure Glycerine Jelly lita 50,Vaseline Petroleum Jelly kilo 44,Pamba 16,Gozi 7 vyote vikiwa na thamani ya shilingi milioni mmoja laki na tisini elfu (1,190,000/=)

 Prof. Ngowi amesema pamoja na vifaa hivyo wanajumuiya hao walichangia damu ili kuokoa maisha ya majeruhi na amewaomba taasisi, mashirika na watu binafsi kutoa msaada wa hali na mali kwani wagonjwa bado wanahitaji msaada , lakini pia   kuwaombea wale waliofariki, wauguzi pia  wanahitaji msaada ili kuwatia moyo , pengine hata msaada wa kisaikolojia hivyo wataalamu wa saikolojia watoe msaada katika eneo hilo.

 Akipokea Msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru, Mfamasia Mkuu wa Hosptalini ya Taifa Muhimbili Dkt. Deus Buma amesema  msaada huo wa vifaa tiba unafaa kwa wagonjwa hasa wa majeraha ya moto na umefika kwa wakati husika.

  “Tunawashukuru kwa msaada mliotupatia unafaa kwa wangojwa moja kwa moja, kwani vifaa kama glycerine na vaseline zinatumika kutengenezea blanketi kwa ajili ya  kufunika katika vindonda kwa majeruhi wa moto” amesisitiza Dkt. Buma.

Dkt. Buma alisema  wanakaribisha wato wote wenye mapenzi mema kuendelea kutoa misaada kwani bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa tiba kwa magonjwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

PICHA YA JUU: Mkuu wa Kampasi  Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Prosper Ngowi (katikati) akisisitiza jambo baada ya kukabidhi vifaa tiba.

 

PICHA JUU:Mkuu wa Kampasi  Dar es Salaam ya Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Prosper Ngowi (wa pili kushoto) akiwa na baadhi ya wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe.

 

P

PICHA JUU:Wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe wakipata maelekezo kutoka kwa Mfamasia Mkuu wa  Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Deus Buma, muda mfupi kabla ya kupokea msaada wa vifaa tiba kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.

 

PICHA:Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Deus Buma,(wa tatu kutoka  kulia) akiwaongoza eneo la bohari, wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kwa ajili ya kupokea msaada wa vifaa tiba vivivyochangwa na wanajumuiya hao.

 

 

 

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. || This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

About us

Social Connect