The Directorate of Research, Publications and Postgraduate Studies (DRPS), Mzumbe University invites applications for admission to the postgraduate programmes (Masters and Doctoral degree Programmes) for the 2023/2024 academic year from qualified candidates.

A: MASTER’S DEGREE PROGRAMMES

Master’s degree programmes are offered at three campuses: the Main Campus (Mzumbe, Morogoro), Dar es Salaam Campus (at Upanga, Dar es Salaam City) and Mbeya Campus (at Forest, Mbeya City). All programmes offered at Mzumbe Main Campus are fulltime, day sessions mode and residential but due to limited accommodation, some successful applicants may be required to seek for alternative accommodation off campus. The Dar es Salaam Campus offers day, evening, and executive mode classes, while the executive mode is for MBA and MPA programmes only. Mbeya Campus offers evening mode classes only. Both Dar Es Salaam and Mbeya Campuses do not have accommodation arrangements for the students, they are non-residential.

THE DEADLINE FOR SUBMITTING APPLICATION FOR MASTER’S DEGREE PRGRAMMES IS 29TH OCTOBER, 2023.

 

For more details, Click here

 

For Non- Degree Programmes offered at Main Campus Morogoro and Mbeya Campus, Click here

 

CLICK HERE TO APPLY

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Taaluma, Utafiti na Ushauri, wakati wa warsha ya mafunzo, Dkt. Nsubiri Isaga, amepongeza na kushukuru chuo cha Pretoria kuchagua kufanya kazi na Mzumbe na kuwataka  wanafunzi kujiandaa vizuri na kufanya bidii katika masomo, ili kupata ufaulu mzuri, utakaowawezesha kukidhi vigezo vya kupata ufadhili wa masomo nje ya nchi.

Akielezea namna walivyojipanga katika kupata wanafunzi wenye sifa, Dkt. Grace Ramafi,  Mhadhiri na Mkuu wa Kitengo cha “Mastercard Foundation Scholars Program” kutoka chuo cha Pretoria, amesema wamejikita katika kutafiti, kutathimini na kuwajengea uwezo wanafunzi ili waweze kupata kwa urahisi ufadhili wa masomo katika ngazi ya shahada za awali na umahiri unaotolewa na Chuo hicho.

Aidha ameongeza kuwa, Chuo Kikuu Mzumbe kimekuwa ni chaguo bora katika kuimarisha ushirikiano wa fursa mbalimbali kutokana na ubobevu na taaluma bora zinayotolewa na Chuo Kikuu Mzumbe.

Dkt. Lucy Massoi, Kaimu Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa na Baraza la Wahitimu,  amesema wamejizatiti vyema katika kuhakikisha ushirikiano bora unaendelea kuimarishwa kati ya vyuo hivyo, pamoja na kuwahimiza wanafunzi wa Mzumbe kuchangamkia fursa ya kuomba nafasi za masomo na ufadhili zilizotolewa kupitia mpango wa “Mastercard foundation Scholars Program”.

Mpango huo umeanza kwa warsha ya siku moja na mafunzo kwa wanafunzi na wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro, kuwapa mwongozo na taratibu za kuomba nafasi hizo.

 

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta amefanya ziara ya kikazi Kampasi ya Dar es Salaam na kupongeza jitihada kubwa zilizofanyika za kupandisha hadhi Kampasi hiyo kuwa Ndaki “Campus College”.

 Katika ziara hivyo Mhe. Samatta aliongozana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza CPA. Pius Maneno, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof Lughano Kusiluka na wajumbe wa Menejimenti; na kuzungumza na Wafanyakazi, Wanafunzi na kukagua maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu Tegeta, eneo ambalo limeandaliwa kwa ajili ya masomo ya Shahada za Kwanza mwaka wa masomo 2020/2021.

 Akizungumza mara baada ya kukagua miundombinu ya Chuo hicho, Mhe. Samatta ameupongeza uongozi kwa jitihada na mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya muda mfupi Tegeta, akilinganisha na taswira aliyoiacha wakati alipofanya ziara yake ya mwisho mwaka jana 2019. 

 “Nimefarijika sana kuona mabadiliko haya makubwa kwakweli sikutegemea. Ila nina imani kubwa kituo hiki kitafungua fursa nyingi na kuongeza idadi ya wananchi wanaotaka kujiendeleza na Elimu ya Juu, kwakuwa hapo awali walilazimika kwenda kufuata masomo ya shahada za awali kwenye Kampasi zetu Morogoro au Mbeya…” akisisitiza 

 Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Profesa Lughano Kusiluka, amesema tayari Chuo kimeshapata idhini ya kuanzisha kozi za awali Tegeta kutoka Tume ya Vyuo Vikuu(TCU) na kwamba wanaendelea na hatua za mwisho za maandalizi ya  miundombinu kwaajili ya kupokea wanafunzi kwa mwaka ujao wa masomo na kwa kuanza wataanza na kozi mbili  za awali ambazo ni Shahada ya Utawala wa Umma (Bachelor of Public Administration -BPA) na Shahada ya Uhasibu na Fedha- Sekta ya Biashara (Bachelor of Accountancy and Finance- Business Sector (BAF-BS).

 Ziara ya Mkuu wa Chuo Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta ni sehemu ya utaratibu aliojiwekea kila mwaka wa kutembelea Kampasi zote zilizopo chini ya Chuo hicho, kukagua shughuli na miradi ya maendeleo, kuzungumza na Wafanyakazi na Wanafunzi,  pamoja na kujibu hoja mbalimbali.

 Hii ni ziara yake ya mwisho kufuatia muda wake wa uongozi kufikia tamati ambapo tarehe 13 Januari 2021 atakuwa ametimiza miaka 11 ya uongozi wake tangu alipoteuliwa mwaka 2009 na Rais wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kushika wadhifa huo.

 Dar es Salaam Campus College offers two Barchelor Degree Programmes:

      1. Bachelor of Accounting and Finance in Bussiness Sector(BAF-BS)

      2. Bachelor of Public Administration( BPA)

 

Click here For more Details about these Programmes.

Chuo Kikuu Mzumbe kwa kushirikiana na Taasisi ya  Kuehne Foundation ya Uswis wanaendesha mafunzo ya siku tatu ya manunuzi na ugavi kwa watendaji wa Serikali, Mashirika na Taasisi binafsi, yaliyoanza Jumatano Julai 15, 2020 katika Kampasi ya Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mkuu wa Kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Honest Ngowi, amesema mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wataalam hao ili kuendana na mabadiliko duniani ya kufanya Ugavi na manunuzi kidigitali.

“ lengo letu Chuo Kikuu Mzumbe ni kuwawezesha wataalamu wetu kuendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia duniani na malengo ya milenia ya kuwa na uelewa wa pamoja katika masuala yanayohusu mifumo ya ugavi kwa kutumia teknolojia. Lengo ni kuwezesha shughuli nyingi za kibiashara kufanyika kidijitali." Alisisitiza   

Kwa upande wa Mwakilishi Mkazi wa Taasisi la Kuehne Foundation, Beatrice  Millu,  amesema kuwa taasisi yake inafanya kazi kwa karibu na Taasisi zenye kutoa ujuzi ili kusaidia Wakufunzi na wanataaluma kuwa na uelewa wa kutosha katika masuala ya mnyororo wa manunuzi na ugavi hapa nchini.

"Ili kuweza kuboresha shughuli za ugavi na manunuzi  hapa nchini  Taasisi yetu iliamua kushirikiana na Chuo Kikuu Mzumbe ili kuwafikia wadau wengi zaidi kwenye mashirika, taasisi za umma na binafsi, na tunafarijika kuona tumefanikiwa kwenye hili ” Alisema Bi. Millu. 

Naye Mratibu wa mradi huo kwa upande wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Omary Swalehe amesema wameandaa mafunzo hayo kwa lengo la kuwaandaa  wataalamu wa manunuzi na ugavi kuendana na mahitaji ya sasa ya  taaluma ya Mnyororo wa ugavi na manunuzi, ambayo imejikita zaidi katika matumizi ya  Teknolojia.

                                                             **************************************************************************

Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya Kuehne Foundation Bi, Beatrice Millu  wa (kwanza kushoto) akifatilia mada akiwa na washiriki wengine katika mafunzo ya siku tatu ya iliyoshirikisha wataalamu wa sekta ya Ugavi na Manunuzi yanayoendelea katika Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam.

Mratibu wa  Kuehne Foundation wa Chuo kikuu mzumbe, Dkt. Omary Swalehe , akizungumza  akisisitiza jambo wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatau yanayoendelea katika Chuo hapo.

Baadhi ya washiriki wa mafunzo wakifatitia mada

Waandaaji na washiriki wa mafunzo wakiwa katika picha ya kumbumkumbu

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. || This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.

About us

Social Connect