MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU MZUMBE PROF. WILLIAM MWEGOHA AENDELEA NA ZIARA YA KIKAZI NDAKI YA DAR ES SALAAM

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, ameendelea na ziara yake ya kikazi ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Ndaki ya Dar es Salaam katika Kituo cha  Shahada za Awali kilichopo Tegeta, pamoja na kuzungumza na wafanyakazi.

Akiwa katika Kituo cha Tegeta Prof. Mwegoha alitembelea na  kukagua miuondombinu ya barabara, ujenzi wa viwanja vya michezo, majengo ya madarasa pamoja na kukagua viwanja vya Chuo vilivyopo eneo la Mbweni jijini dar es salaam, na kuhimiza watendaji wanaohusika na usimamizi wa miradi hiyo kuongeza kasi ili miradi iliyobuniwa kukamilika kwa wakati..

Aidha, amesisitiza wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kuwa waadilifu na  waaminifu kwa kuzingatia nidhamu ya kazi kama watumishi wa Umma; kufuata taratibu, sheria, kanuni na miongozo iliyopo katika utumishi wa umma. 

Katika ziara hiyo, Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo aliambatana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Allen Mushi,  Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Huduma za Jamii Dkt. Elizabeth Mwakasangula na viongozi wengine waandamizi wa chuo hicho.  

Mwegoha, akiwa ameambatana na na Menejimenti ya Chuo wakati wa kukagua maeneo mbalimbali ya Kituo cha Tegeta.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miliki na Majengo, Msanifu Majengo Joseph Ng’wala, akitoa taarifa kwa Kaimu Makamu Mkuu wa

Chuo, Prof. William Mwegoha kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kituo cha Tegeta.

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, akizungumza na Menejimenti ya Chuo Kikuu Mzumbe katika Kituo cha Tegeta

mara baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya kituo hicho kutoka kwa Mratibu wa Kituo Profesa Felician Barongo.

Wafanyakazi wakimsikiliza kwa makini Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo wakati wa kikao na wafanyakazi

Wafanyakazi wa kituo cha Tegeta wakiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu Mzumbe.

 

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

About us

Social Connect