MAKAMU MKUU WA CHUO KIKUU MZUMBE ATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha, ametembelea na kukagua maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro, ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu alipoteuliwa kukaimu nafasi hiyo.

Prof.Mwegoha, ameridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo, na kusisitiza watumishi wanaotekeleza miradi hiyo kuongeza kasi na  kuzingatia utaalamu, ikiwa ni pamoja na kutumia fedha kulingana na bajeti iliyoidhinishwa ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kuleta tija iliyokusudiwa.

Katika ziara hiyo kaimu Makamu Mkuu wa chuo aliambatana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Mipango, Fedha na Utawala,  Prof. Allen Mushi, Wajumbe wa Menejimenti na wataalamu wa Kitengo cha miliki na majengo wenye dhamana ya kusimamia miradi hiyo.

***************************************************

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Miliki na Majengo, Arch. Joseph Ng’wala, akitoa taarifa kwa Kaimu Makamu Mkuu

wa Chuo, Prof. William Mwegoha (katikati), kuhusu maendeleo ya ukarabati wa kiwanja cha michezo Kampasi Kuu Morogoro

Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Prof. William Mwegoha (wa nne Kushoto) akijadiliana na wataalamu mara baada ya kukagua ukarabati wa jengo la kusomea kwa wanafaunzi wa Shahada ya uzamivu (PhD).

Prof. William Mwegoha, akitazama ukarabati unaoendelea katika jengo la Maktaba Kuu ya Chuo Kikuu Mzumbe, Kampasi Kuu Morogoro.

Ukaguzi ukiendelea wa maandalizi ya eneo yatakapofanyika Mahafali ya 21 ya Chuo Kikuu Mzumbe  kampasi  Kuu Morogoro.

Prof. Mwegoha akikagua maandalizi yanayofanyika eneo litakapojengwa jengo jipya la Utawala katika eneo la Maekani Kampasi Kuu Morogoro.

Mradi huo utaanza utekelezaji hivi karibuni.

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

About us

Social Connect