MUSO-DCC WAPATA VIONGOZI WAPYA

CHUO Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam kimewaapisha Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi (MUSO DCC) ambao wameshinda katika uchaguzi wa Viongozi mara baada ya Uongozi Uliopita Kumaliza Muda wake. Uchaguzi huo katika ndaki ya Dar es Salaam, ulifanyika Mei, 26,2022 katika Kituo Cha Tegeta na Upanga.Viongozi hao wapya wataongoza kwa Mwaka Mmoja wa 2022/2023 ambapo watamaliza muda wao.

Walioapishwa leo ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSO DCC), Ombeni Kisuka aliyeshinda kwa kura 135 baada ya kuwashinda Carren Njogoro na Abdallah Omar.Na katika nafasi ya Makamu wa Rais, Zauda Halisi ameshika nafasi hiyo baada ya Mgombea wa Urais Kisuka kuibuka Mshindi. Katika nafasi ya Mwakilishi wa Seneti, Zephani Malembele ameapishwa mara baada ya kushinda nafasi hiyo kwa kura 265.

 Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba akizungumza mara baada ya kuapishwa amewaasa kuongoza huku wakijua kuwa wao ni Wanachuo.Amesema kuwa kiongozi mzuri ni yule ambaye anafaulu mitihani Vizuri bila kuwa na kipolo katika mitihani pia amewaasa kushirikiana na Viongozi wengine wa chuo ili kuleta maendeleo yenye tija kwa jamii nzima wa Wanamzumbe.

 Kwa Upande wa Mwanasheria kutoka Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Nora Msuya amewasisitiza viongozi wapya kufata misingi ya uongozi kwani katika kuongoza wanafunzi wenzao kwani katika kuongoza ndio mwanzo wa kuwa viongozi wazuri au wabaya hivyo wanatakiwa waadilifu katika kipindi cha uongozi wao.

 “Nina imani mtapatiwa mafunzo ya uongozi, hivyo basi mnatakiwa kufata misingi ya uongozi mtakayofundishwa pamoja na sheria na miaongozo mtakayopewa mkaitumie vizuri kwani  hatua mliyoifikia ni hatua nzuri mjitahidi huko baadae mje kugombea nafasi za uongozi wa siasa serikalini.”Alisisistiza Dkt. Msuya

 Kwa Upande wa Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSODCC), Ombeni Kisuka amesema uongozi wake utakuwa wa kushirikisha kati ya wanafunzi, Viongozi wa chuo na Viongozi wa MUSO.

 Aidha Rais wa Serikali ya wanafunzi aliyemaliza muda wake, Jonas Baraka amewapongeza kwa kuchanguliwa kwao na watakia mwema katika kuongoza Wanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa wanachuo wengine pale zinapotokea ili kila mwanafunzi awe na taarifa kwa kile kinachoendelea.

 Akiwapongeza Viongozi wa MUSO DCC, mshauri wa Wanafunzi Bi. Zitta Mnyanyi amewapa hongera kwa nafasi waliyoipata pia amewashauri wakaongoze kwa weredi wanafunzi wenzaao bila kuwa na ubaguzi.

*********************************************************************************************************************

Rais wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam (MUSODCC),Ombeni Kisuka akiapishwa na Mwanasheria kutoka Chuo Kikuu Mzumbe,Dkt. Norah Msuya Juni Mosi, 2022.

Rais wa Serikali ya Wanafunzi aliyemaliza Muda wake(MUSODCC), Jonas Baraka akimkabidhi Rais wa Serikali ya Wanafunzi (MUSODCC),baadhi ya nyaraka ambazo zitawaongoza katika kuongoza serikali hiyo ya wanafunzi jijini Dar es Salaam Juni Mosi, 2022.

Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam Dkt. Coretha Komba akizungumza na uongozi mpya wa serikali ya wanafunzi baada ya kuapishwa.

Mwanasheria wa Chuo Kikuu Mzumbe ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Nora Msuya akizungumza mara baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali wa

serikali ya wanafunzo wa Ndaki ya Dar es Salaam (MUSODCC) Juni Mosi, 2022.

Kaimu Mkuu wa Ndaki ya Dar es Salaam, Dkt. Coretha Komba aliyekaa katikati, Rais Ombeni Kisuka kulia na rais

aliyemaliza muda wake Jonas Baraka kushoto wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine wa Serikali ya wanafunzi mara

badaya ya kuapishwa serikali mpya Juni Mosi, 2022.

 

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

About us

Social Connect