WAFANYAKAZI CHUO KIKUU MZUMBE WATOA FARAJA KWA WATOTO WALIOPO MAHABUSU YA UPANGA

 
 WANAWAKE wafanyakazi Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam wametoa msaada wa mahitaji muhimu kwa watoto waliopo mahabusu ya Watoto Upanga, jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwafariji watoto.

 Akizungumza wakati walipotembelea kituo hicho, Mkuu wa Kitengo cha Masomo ya Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge amesema watoto waliopo katika Mahabusu ya Upanga wanatakiwa kupendwa na kujaliwa kama watoto wengine. Chuo Kikuu Mzumbe kuwasaidia watoto waliopo katika Mahabusu ya Watoto Upanga kutimiza ndoto na kutoa elimu ya biashara.

Akizungumza wakati walipotembelea Mahabusu hiyo Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Honest Ngowi, amesema kuwa watoto wengi wamesema malengo yao ni kuwa wafanyabiashara mbalimbali hivyo kama chuo watapanga ratiba kwa ajili ya kuwapa elimu ya biashara watoto walio katika mahabusu hiyo.
 Kwa upande wake Meneja wa Mahabusu ya Watoto - Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo amesema kuwa watoto waliopo katika mahabusu hiyo wanaweza kila kitu wanachofundishwa na walezi wao, hivyo wanabadilika kila siku kutokana na ushauri wanaupata.
Amesema watoto waliopo katika Mahabusu hiyo wanafundishwa mambo mbalimbali ikiwemo msaada wa kisaikolojia pamoja na kupewa Upendo, Kutambuliwa, kupewa usalama, Kukubalika, Kusifiwa pale wanapofanya vizuri, Kuheshimiwa, Kushirikishwa, Kuaminiwa, Kulindwa na kupewa fursa ya Kucheza.
 
                                                                      *************************************
Mkuu wa Idara Masomo ya Utawala, Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam, Mary Rutenge, akimkabidhi Meneja wa Mahabusu ya Watoto - Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Darius Kalijongo baadhi yavitu vilivyotolewa na wanawake wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam. Kulia ni Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Honest Ngowi.
 
 
 
 
 

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

About us

Social Connect