ZIARA YA DKT. ALI MOHAMED SHEIN

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amekamilisha ziara yake ya kutembelea Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuzungumza na wafanyakazi wa Ndaki ya Dar es Salaam.

 Mheshimiwa Dkt. Shein ambaye alisimikwa rasmi Januari 5,2021 kuwaMkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe akiwa katika ziara hiyo alipata taarifa ya miradi ya maendeleo ya Ndaki ya Dar es Salaam na kutembelea Kituo cha kinachofundisha Shahada ya kwanza kilichopo Tegeta- kwa Ndevu.

Akiwa katika kituo cha Tegeta alizungumza na wanafunzi wanaondelea na masomo katika kituo hicho na kuwasisitizia wasome kwa bidi kwani taifa linawahitaji wasomi watakao tumika katika maslahi mapana ya nchi.

“Hakuna njia ya mkato kuzifikia ndoto zenu na taifa linawahitaji katika kutumika katika maslahi ya nchi jitahidini msishindwe, neno kushindwa liwe aibu kwenu hakuna aliyezaliwa na kila kitu na mjitahidi kusoma hakuna njia ya mkato katika maisha.” Alisisitiza Dkt Shein

Katika ziara hiyo Dkt. Shein aliambatana na viongozi mbali mbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Abubakar Kunenge, Mkuu wa wilaya Kinondoni Mhe. Daniel Chongolo na viongozi Serikali ya Mtaa wa Tegeta.

Alimaliza ziara yake ya kutambulishwa kwa kupanda mti wa kumbukumbu katika kituo hicho cha Tegeta.

 

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam Upanga.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akipokelewa na Mratibu wa Ndaki ya Dar es Salaam Chuo Kikuu Mzumbe Kituo cha Tegeta, Dkt. Omary Swalehe.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe na Rais Mstaafu wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na wanajumuiya wa Chuo Kikuu Mzumbe.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Abubakar Kunenge akikisisitiza jambo alipokuwa akiwasalimia wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe Ndaki ya Dar es Salaam.

Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akifafanua jambo kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein alipotembelea Maktaba iliyopo kituo cha Tegeta.

Rasi wa Ndaki ya Dar es Salaam, Prof. Honest Ngowi, akifafanua jambo kwa Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein alipotembelea 'Computer lab' iliyopo kituo cha Tegeta.

Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Ali Mohamed Shein, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abubakar Kunenge wapili kutoka kulia wakiwa katika picha ya Pamoja na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu Mzumbe pamoja na Menejimenti ya Ndaki ya Dar es Salaam.

 

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

About us

Social Connect