ZIARA YA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU,SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe amehitimisha ziara yake Chuo Kikuu Mzumbe kwa kutembelea na kukagua ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya Kampasi ya Dar-es-salaam Tegeta ambacho kimekusudiwa kuanza kutoa  Shahada za Awali kwa mwaka 2020/2021

 Aidha, amepongeza hatua kubwa iliyofikiwa hadi sasa katika ujenzi wa vyumba za madarasa na mihadhara na   kupendekeza ujenzi unaoendelea kuendana na mahitaji ya sasa ya mabadiliko ya teknolojia, kwa kuwezesha matumizi ya teknolojia katika ufundishaji.

 Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Naibu Makamu Mkuu Chuo Prof Ernest Kihanga amesema ukarabati huo ulianza Juni 2018 ukiwa ni upanuzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam na kwamba ujenzi umekamilika kwa asilimia 99, na majengo yako tayari kuanza  kutumika pindi idhini ya Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) itakapotolewa.

 Amesema chuo hicho kitakuwa na maktaba, ofisi za walimu, vyumba vya madarasa na mihadhara, vyumba cha komputa na huduma nyinginezo muhimu kumwezesha mwanafunzi kusoma. 

 Kuanzishwa kwa programu za Shahada za awali kwa Kampasi ya Dar-es-Salaam kutaongeza wigo wa vijana wengi zaidi kujiunga Na elimu ya juu nchini sambamba  na kuongeza fursa za ajira.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akisaini kitabu cha wageni mara bada ya kuwasiri katika Chuo kikuu cha Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam-Tegeta, kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ukarabati na ujenzi wa Vyumba vya madarasa.

 

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe (Utawala na Fedha) akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa upanuzi wa Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam Tegeta Dar es Salaam  kwa Naibu Katibu Mkuu wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi.

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akiwa ameabatana na wafanyakazi wa chuo kikuu cha mzumbe wakitembelea majengo ya  chuo kikuu cha Mzumbe jijini Dar es Salaam leo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe akikagua  moja ya madarasa ya Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam Tegeta Dar es salaam ambako Shahada za Awali yanaterajiwa kuanza.

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe (Utawala na Fedha) Profesa Ernest Kihanga akitoa maelekezo kwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa James Mdoe wakati alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya Kikuu cha Mzumbe- Tegeta jijini Dar es Salaam.

 

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

About us

Social Connect