CHUO KIKUU MZUMBE WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KWA KUWAFUNDA WASICHANA

Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kimeadhimisha siku ya Wanawake Duniani kwa kuwafunda watoto wa kike katika shule ya Sekondari ya Hananasif jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanafunzi wa hao siku ya kilele cha maadhimisho hayo; Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo hicho Dkt. Godbertha Kinyondo amesema wasichana hawana budi kujiamini ili kufikia malengo yao ya baadaye.

Amewataka vijana wa kike kujiamini na kushiriki kikamilifu katika fursa mbalimbali zinazotolewa kwa vijana hasa watoto wa kike.

“Zipo fursa nyingi kwa vijana hasa wa kike, zinazotolewa kwa vijana ambazo zitawajenga kuwa na  uthubutu wa ushiriki wa mambo mbalimbali ya kitaifa na kimataifa” alisisitiza Dkt Kinyondo.

Mwanasheria na mjasiliamari, Bi Vicensia Fuko ameeleza changamoto mbalimbali wanakokumbana nazo watoto wa kike na kuwataka  wazazi kuwa karibu zaidi na watoto wao badala ya kuwa wakali na hivyo kupelekea watoto kushindwa kueleza changamoto wanazokutananazo katika maisha.

Mwanafunzi wa Kidato cha Pili wa Shule hiyo ameiomba Serikali na Taasisi mbalimbali kuangalia jinsi ya kuwafikia na kuwaelimisha wasichana mbinu za kukabiliana na changamoto mbalimbalina hasa vitendo vya kikatili vinavyofanywa na jamii inayowazunguka.

“watoto hatujui tukamweleze nani matatizo yetu, vitisho ni vingi na hatuna mtetezi , wadogo zetu wanafanyiwa vitendo vya ukatili na hawawezi kumkimbilia mzazi kutokana na vitisho na wakati mwingine aliyemtendea ni mtu wa nyumbani kwao. ” alisisiza

Kongamano hilo lilifunguliwa na Dkt Faisal Issa Mkuu wa Idara ya Kozi Fupi na Shauri za Kitaalam kwa  niaba ya Mkuu wa Kampasi ya Dar es salaam ambaye amesema Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam kitaendelea kushirikiana na jamii kwa kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali katika jamii katika nyanja zote ikiwemo uchumi.

Mkuu wa Idara ya Kozi Fupi na Shauri za Kitaalam Dkt. Faisal Issa kwa niaba  Mkuu wa kampasi ya Dar es Salaam akiwakaribisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Hananasif jijini Dar es Salaam katika kuadhimisho Siku ya Wanawake Duniani yaliyoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam Machi 7, 2020. Kauli mbiu “Kizazi cha Usawa kwa Maendeleo ya Tanzania ya sasa na ya baadae”

Mwanasheria na mjasiliamali, Vicensia Fuko akizungumza na wanafunzi  wa Shule ya Sekondari Hananasif  wavunje ukimya na wanapokumbana na vitendo vya kutaka kukatisha ndoto zao kwa maendelea ya taifa.

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Hananasif ya jijini Dar es Salaam wakifiatilia mada zinazotolewa.

Mkuu wa Idara ya Kozi Fupi na Shauri za Kitaalam Dkt. Faisal Issa (katikati), Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Mzumbe Dkt. Godbertha Kinyondo (Kushoto) na Mwl.  Tatu Mayeye  (Kulia) katika picha ya pamoja na wanafunzi wakike wa Shule ya Sekondari Hananasif Manispaa ya Kinondoni walipohudhuria Kongamano la siku ya Wanawake Duniani lililoandaliwa na Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi ya Dar es Salaam mwishoni wa juma Upanga Dar es salaam.

 

 

Address

Mzumbe University,
Dar es Salaam Campus College,
Upanga Area Plot No. 941/2 Olympio Street,
P.O.Box 20266, Dar es Salaam, Tanzania
General Line: +255 (0) 22 2152582,
Direct Line: +255 (0) 22 2152586,
Fax: +255 (0) 22 2152584/2150398,
Cell: +255 (0) 689 455 588,
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

About us

Social Connect